Unajua imekuwa hii ni ishu ambayo inakaa
sana kwenye headlines, upande wa Bongo Sheria zimebanwa zaidi kuzuia
matumizi ya dawa za kulevya, Marekani tukasikia story tofauti, wao kuna
Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi
kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa
nyingine Majimbo kama ya Washington DC, Alaska.
Hii ya leo ni kwamba Jimbo la Colorado unaambiwa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 (zaidi ya Bil. 27 Tshs).
Fungu hilo la kodi linapelekwa kujenga
Shule mbalimbali kupitia mpango wa Jimbo hilo uliopewa jina la Building
Excellent Schools Today (BEST)
Tangu kupitishwa utaratibu wa kuruhusu
uuzaji wa bangi, unaambiwa maduka ya kuuza bidhaa hiyo rejareja mtaani
kuanzia Jan. 1, 2014 mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni
dola Mil. 15 ambazo zinasaidia kuboresha mazingira ya Shule za Umma
katika Jimbo hilo.
Kwako mtu wangu, unadhani itakuwa sawa nchi za Afrika nazo waruhusu bangi ili kuongeza mapato ya kodi?
No comments:
Post a Comment